Antoine Griezmann atua rasmi Barcelona


Alikyekua mshambuliaji wa Atlentico Madrid , Antoine Griezmann amekamilisha rasmi usajili wake kwenda klabu ya Barcelona baada ya makubaliano ya uhamisho wa paundi milioni 108 sawa na kama bilioni 300 za kitanzania .

Griezmann alitua jijini Barcelona siku ya ijumaa ambapo alitembezwa kwenye duka ya klabu hiyo na kuonyshwa jezi yenye jina lake mgongoni .

“Nina furaha sana na nategemea kufanya kazi na kikosi kizima na kukutana na wachezaji wenzangu . ‘Ni changamoto mpya , yenye malengo mapya , nategemea nitafanya vizuri pia kama ilivyokua kwenye klabu niliyoondoka na kikosi cha taifa . Kuna malengo ya klabu na yangu binafsi nategemea kuyatimiza yote .”

Furaha nyingine aliyonayo Griezmann ni kucheza na Lionel Messi . Aliendelea kusema : ” Nategemea kumuona alivyo siku hadi siku , kwenye mazoezi , kucheza pamoja naye ni furaha isiyo na kifani . ”

Griezmann alitangaza kuachana na klabu ya Atlentico Madrid Tarehe 14 mwezi wa 5 baada ya kucheza misimu mitano na klabu hiyo .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com