Azam FC yatoshana nguvu na Jamhuri Mapinduzi Cup..


Klabu ya Azam FC imeanza mbio za kutetea taji la Mapinduzi Cup kwa kutoka sare ya bao 1-1  dhidi  Jamhuri ya Pemba katika mchezo uliopigwa jana , Jumatano usiku katika dimba la Amaan .

Bao la kwanza la Azam FC walilipata dakika ya 28 ya mchezo kupitia kwa Raphael Kutinyu.

Hadi kipindi cha Kwanza kinamalizika , Azam FC walikua mbele kwa bao 1 – 0 . Kipindi cha pili , dakika ya 66 , Jamhuri walijipatia bao la kusawazisha kutoka kwa Abdul Yusuf Ramadhan aliyetokea benchi .

Safu ya ushambuliaji ya Azam FC iliongozwa na Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Kutinyu ambapo Kutinyu na Ngoma walitolewa na nafasi zao kuchukuliwa na Salimin Hoza na Abdul Abdallah.

Baada ya mchezo huo Kocha wa Azam FC ameeleza kusikitishwa na kusema kuwa huu ulikuwa ni mchezo wa wao kushinda hivyo amesikitishwa na wachezaji wake “Kuhusu kiwango kilichooneshwa na timu nimesikitishwa kiukweli kwa kawaida ulitakiwa kusuhinda hii mechi kama usiposhinda lazima usikitishwe”

Timu hizo za Kundi B zitakutana na wapinzani wao wengine ambao ni Yanga,  KVZ na Malindi.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com