Azam VS Stand United na matokeo yote ya mechi za leo


AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada kuwalaza mabao 2-0 wenyeji Stand United Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jioni ya leo. Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, mshambuliaji wa Kenya, Alan Watende Wanga na kiungo mzalendo Frank Rymond Domayo. Huo ushindi wa pili mfululizo kwa Azam FC ya kocha Muingereza Stewart Hall, baada ya awali kuichapa Prisons ya Mbeya 2-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Azam-vs-Tanzania-Prisons-bngosoka

Katika mchezo mwingine JKT Ruvu wameendeleza jinamizi la kupoteza mchezo baada ya leo kukubali kichapo cha pili mfululizo toka kwa Mbeya city, ambayo nayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza. Katika mchezo wa leo Mbeya city walianza kuandika goli lao la kwanza katika dakika ya 25 kupitia kwa Joseph Mahundi goli liliowapeleka Mbeya City mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0. Katika kipindi cha pili Mbeya city walifanikiwa kufunga magoli mawili yaliyofungwa na Themi Felix katika dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati, na jingine kupitia David Kabole katika dakika ya 68. Mpaka dakika 90 zinakamilika Mbeya city walikuwa mbele kwa goli 3-0 na kufanikiwa kujikusanyia pointi zake tatu katika uwanja wake wa Sokoine ya Mbeya.

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO
MAJIMAJI 1-0 KAGERA SUGAR
NDANDA FC 1-0 COASTAL UNION
YANGA 3-0 T.PRISONS
MGAMBO SHOOTING 0-2 SIMBA SC
TOTO AFRICANS 1-2 MTIBWA SUGAR
MWADUI FC 2-0 AFRICAN SPORTS
STAND UNITED 0-2 AZAM FC
MBEYA CITY 3-0 JKT RUVU

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com