Baada ya Ajib na Gadiel, TSHISHIMBI nae kutua Simba…


Imeripotiwa kwamba, klabu ya soka ya Simba iko katika nafasi ya nzuri ya kumtwaa kiungo mkabaji na nahodha wa klabu ya soka ya Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi ambaye amekuwa katika kiwango kizuri kwa sasa ndani ya klabu hiyo.

Papy Kabamba Tshishimbi kazini.

Ikumbukwe kwamba mkataba wa Tshishimbi ndani ya Yanga unamalizika msimu huu na baada ya hapo atakuwa huru kujiunga na klabu yoyote.

Picha nzima iko hivi…

Mazungumzo ya klabu ya Yanga na kiungo wao anaemaliza makataba Papy Tshishimbi yamegonga Mwamba kutokana na matakwa ya mchezaji huyo kuwashinda mabosi wa klabu hiyo .

Taarifa zinasema Tshishimbi amewaambia Yanga ili asaini makataba mpya waweke mezani mshahara wa shilingi Milion 18 kwa mwezi na hela ya Usajili milioni 150 huku Yanga wakimjibu hapo hapo kuwa hawataweza kutokana na umri wa mchezaji huyo kusogea (miaka 30) .

Inasemekana Yanga wamemwambia Tshishimbi wako tayari kumpa nusu ya Mshahara alioutaka (milioni 9 kwa mwezi) na nusu ya milion 150 kama pesa ya Usajili (milioni 75), mbali na hapo wamemtakia maisha mema huko aendako kwani mkataba wake unamalizika mwishoni wa msimu huu.

Moja ya vilabu ambapo inatajwa kuwa ni Simba sc, tayari vimefanya mazungumzo ya awali na Tshishimbi na wameahidi kumpa kile anachokitaka.

Tshishimbi mwenyewe afunguka…

“Mtu akija kuongea na mimi mkataba, ninajua nitaanzia wapi na nitaishia wapi nakutajia bei yangu nakusikiliza na wewe unasemaje,” alisema Tshishimbi mapema leo alipokuwa akiongea ktk kupitia kipindi cha michezo cha redio EFm.

” Lakini kama nakutajia yangu, wewe unakaa kimya, nifanyaje ?…. NAONDOKA ZANGU,” aliongeza Tshishimbi.

Huenda msimu ujao Tshishimbi akachezea timu tofauti na Yanga kwenye ligi kuu ya Tanzania bara na pengine timu hiyo ikawa Simba kama ilivyokuwa kwa Ibrahim Ajib na Gadiel Michael, ambao wao walihamia hapo kutoka Yanga msimu huu.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com