CAF kuamua hatma ya wachezaji wapya Yanga


SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limesema kuwa hatima ya Hassan Ramadhan ‘Kessy’, Juma Mahadhi, Benno Kakolanya na Andrew Vincent ‘Dante’ kuichezea Yanga kwenye mechi ya Kundi A, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia itajulikana saa 24 kabla ya pambano hilo.

Taarifa za uhakika  kutoka klabuni humo zinadai kuwa licha ya Yanga kuwasilisha mapema majina ya wachezaji hao CAF, lakini Shirikisho hilo limedai kuwa mbivu na mbichi zitajulikana saa 24 kabla ya mechi ambayo itachezwa Jumapili hii nchini Algeria.

Kikosi-cha-Yanga-Kombe-la-FA-Bongosoka

Inadaiwa kuwa Yanga imepeleka majina hayo manne CAF ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na akina Paul Nonga, Benedict Tinoco, Salum Telela na Mniger Issafou Boubacar, waliotemwa na miamba hiyo ya Jangwani.

Meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh, alilithibitisha  kuwa  tayari wameyawasilisha majina ya wachezaji wote waliowasajili hivi karibuni sasa wanasubiri ruhusa ya CAF ili wawatumie kwenye mechi dhidi ya Mo Bejaia.

Yanga ambao kwa sasa wako nchini Uturuki walikoweka kambi ya wiki moja kujiandaa na pambano hilo la kwanza la hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika, wanahitaji vibali hivyo haraka ili waweze kumtumia Kessy kuziba nafasi ya Juma Abdul aliyebaki nchini kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu (enka) yanayomsumbua.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com