CAF Yapitisha usajili wa Hassan Kessy Yanga


Kwa mara nyingine, Shirikisho la Afrika (CAF) limepitisha usajili wa beki mpya wa Yanga, Hassan Kessy aliyesajiliwa kutoka kwa mahasimu Simba SC.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari , CAF imetoa orodha ya wachezaji wote waliopitishwa katika usajili mdogo wa hatua ya makundi ya michuano ya Afrika – Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

Hassan-Kessy-Yanga-Simba

Na katika Kombe la Shirikisho wachezaji wote wapya watano wa Yanga wamepitishwa na kupewa leseni za kucheza mechi za Kundi A, zinazoelekea ukingoni. Hao ni Obrey Chola Chirwa, Juma Hassan Mahadhi, Benno David Kakolanya, Hassan Khamis Ramadhan ‘Kessy’ na Vicent Andrew Chikupe.

Hata hivyo, kutokana na kosa walilofanya Yanga SC kuanza kumsajili Kessy kabla ya hajamaliza Mkataba wake na Simba, sasa watalazimika kuzungumza na klabu yake hiyo ya zamani ili wamridhie kucheza. Na kwa sababu Yanga imeshindwa kujishusha kwa Simba, Kessy ameendelea kubaki nje huku hatua ya makundi ikielekea ukingoni na timu hiyo ina nafasi finyu ya kusonga mbele.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com