Donald Ngoma amtamani Tambwe


MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma, amesema mashabiki wa klabu hiyo watampenda iwapo kocha wao, Hans Pluijm, atamchezesha na Amis Tambwe kuongoza mashambulizi ya timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani. Ngoma, aliyesajiliwa na Yanga akitokea Klabu ya Platinum ya Zimbabwe, juzi aliifungia Yanga bao pekee katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, ikiwa ni mchezo wake wa kwanza na klabu hiyo mpya. Awali katika mchezo huo, kocha alimpanga Ngoma na Kpah Sherman katika kipindi cha kwanza, lakini kombinesheni yao ilionekana kugoma na baadaye alipoingia Tambwe walionekana kucheza vizuri na hata hali ya mchezo kwa upande wa ushambuliaji ilibadilika.

Hamis-Tambwe-na-Donald-Ngoma-Yanga

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com