draw ya makundi Europa Cup Kufanyika leo , tegemea haya…


Leo , Agosti 26 , Draw ya kuchagua makundi ya Europa League itafanyika katika ukumbi wa Monaco .

Timu 48 zitakazochuana katika hatua ya makundi zitatenganishwa kwenye mafungu manne tofauti huku mpangilio kwenye kila sehemu ukiendana na ushindani wa timu binafsi kwenye ligi ya mabingwa ulaya na Europa Cup kwa miaka 5 iliyopita .

Timu 12 zinazoongoza kwa kiwango zitawekwa kwenye kifungu cha kwanza , 12 zinazofuata kwenye kifungu cha pili , hivyo hivyo hadi kifungu cha nne .

Henry-Europa-League-Draw

Hakuna timu inayoruhusiwa kucheza na timu nyingine inayosimamiwa na chama kimoja cha soka . pia timu kutoka nchi za urusi na ukraine haziruhusiwi kupangwa kwenye kundi moja kwa sababu za kisiasa .

Timu saba zilizotinga kwenye hatua ya makundi mojakwa moja ni wazi kwamba zitawekwa kwenye fungu la kwanza la draw hiyo . Baadhi ya timu kubwa kwenye fungu hilo ni pamoja na Manchester United , Inter Milan na Villarreal.

 

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com