Duh! TP Mazembe yamgeuka Mbwana Samatta


KLABU ya TP Mazembe ni kama imemgeuka straika wa Tanzania, Mbwana Samatta ambaye anataka kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji, hii ni baada ya mmiliki wa mabingwa hao wa Afrika, Moise Katumbi kuvutiwa zaidi na ofa ambayo imetumwa na Standard Liege ya Ubelgiji pia.
Kwa nyakati tofauti Samatta amekuwa akinukuliwa akisema kuwa dili lake la kwenda Genk, limetimia kwa asilimia 90 kwa sababu yeye ameshafanya nao makubaliano binafsi, lakini cha ajabu ni kuwa sasa Katumbi anataka kumuuza Standard Liege ambayo ni klabu tofauti na ile ambayo ilizungumza na Samatta.

Mbwana-Samatta-Taifa-Stars-bongosoka-TP-Mazembe


Hatua hiyo imekuja mara baada ya klabu ya Genk kutokuwa na maelewano mazuri hasa pale Katumbi ambaye anataka kumuuza Samatta kwa euro laki 7.5, lakini klabu hiyo imekomaa kutoa euro laki 5.5 pekee kwa staa huyo wa Tanzania ambaye amebakiza miezi minne tu kwenye mkataba wake wa sasa na Mazembe.


Inaonekana Standard Liege wamepania kuwazidi kete, Genk ndiyo maana wameenda moja kwa moja kwa Katumbi kujaribu kumsajili Samatta ambaye tayari ameshasaini mkataba wa awali na Genk.


Akizungumza  jana, Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema bado Katumbi ameendelea na msimamo wake wa kuwakataa Genk, huku akikomaa kumuuza kwenda Standard Liege ambao ameshaanza mazungumzo nao.


Kisongo alidai kuwa juzi alipokutana na Mwanasheria na Meneja wa TP Mazembe, Fredrick Kitenge walishindwa kufikia mwafaka ambapo jana walikutana tena na kueleza juu ya msimamo wa Katumbi katika Klabu ya Standard.


“Hali halisi inavyoonyesha kwamba Katumbi hahitaji kusikia habari za Genk na tayari ameshaanza mazungumzo na Standard (Liege) hivyo tunahitaji kupata mwafaka kwani tayari Samatta ameshasaini mkataba wa awali na Genk,” alisema Kisongo.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com