Emmanuel Okwi yupo tayari kurudi Simba kwa masharti haya…


Mshambuliaji  nyota wa zamani wa Simba , Emmanuel Okwi, yuko tayari kuondoka Denmark na kujiunga nao tena lakini fedha, ndiyo tatizo kubwa . Okwi amesema yuko tayari  kuondoka  klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu Denmark ili arejee Simba , lakini yeye na klabu hiyo zimetoa masharti kwa Simba.

Sharti la kwanza ambalo wamelipata Simba kutoka kwa klabu hiyo ya Sweden ni kurudishiwa kitita cha dola 120,000 (zaidi ya Sh milioni 250) ambazo walimnunua Okwi kutoka Simba ndani ya miezi sita iliyopita.

“Tumewaambia Simba, Okwi anaweza kuja huko lakini ni lazima waturudishie fedha zetu tulizolipa kumnunua ili wamnunue kumrudisha Dar es Salaam.

Hans-Poppe-okwi--usajili--bongosoka

“Okwi tumezungumza naye na anaonekana yuko tayari kurudi Tanzania, sisi pia hatuna tatizo,” alizungumza mmoja wa maofisa wanaoshughulikia usajili ndani ya Sonderjyske.
Sharti la pili ambalo wamepewa Simba ni kutoka kwa Okwi ambaye amesema kweli yuko tayari kurejea, lakini mshahara apewe dola 5,000 (zaidi ya Sh milioni 12).

Pia ameomba apewe fedha za ada ya usajili kama dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 70), jambo ambalo Simba wamelazimika kufanya mkutano wa dharura ambao ulifanyika jana jioni lengo ni kufikia uamuzi wa hilo, kwamba je, wavunje benki kumrudisha Mganda huyo matata uwanjani?

Taarifa zinaeleza, Okwi ambaye ameoa hivi karibuni, hajawa na furaha aliyoitarajia akiwa na Sonderjyske.

Lakini hata mkewe bado anaonekana kutofurahia maisha ya Denmark na akirejea Uganda, anakuwa mbali na mumewe jambo linalozidisha upweke wa Okwi ughaibuni.
Hivyo, Okwi akaona bora kurejea Afrika na timu ya kwanza kuieleza ikawa ni Simba na Sonderjyske.

 

Alipotafutwa Rais wa Simba, Evans Aveva , hakutaka kulifafanua kwa undani suala hili “Nani kakuambia suala hilo, unajua Simba ni taasisi, hivyo ningependa kwanza mambo yashughulikiwe kabla ya kuanza kutangazwa.”

Iwapo Simba itampata Mganda huyo kwa mara nyingine, bado watakuwa na nafasi kwa kuwa imeacha wachezaji wawili, Simon Sserunkuma na Pape N’daw na imemrejesha Mkenya Paul Kiongera.

Hii itakuwa bahati kwa Simba na sasa itakuwa vigumu kwa Yanga na Azam kupata ushindi dhidi ya vijana hao wa Msimbazi kirahisi kwa kuwa anafahamika kuwa ni mshambuliaji bora sana hapa Afrika Mashariki na Kati.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com