Sio Rasmi : Fedha za okwi zampeleka rumande Evans Aveva


Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva yupo chini ya ulinzi wa Polisi ikiwa ni maelekezo kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) ili kupisha uchunguzi wa masuala yanayoshughulikiwa na Taasisi hiyo .

Taarifa zilizotoka ni kwamba Aveva anashikiliwa katika kituo cha polisi cha urafiki na Taarifa hizo zimethibitishwa na Kamanda Christopher  Foime, ambaye ni Mkuu wa polisi mkoa wa kipolisi  kinondoni.

Simba-mauzo-ya-Emmanuel-Okwi-Bongosoka

Kamanda Faime amesema kuwa Aveva anashikiliwa tangia juzi kwa amri iliyotolewa na TAKUKURU. “Yupo chini ya ulinzi kwa uchunguzi wa masuala hayo ya rushwa na sisi tukiletewa mtu na TAKUKURU tunatimiza wajibu wa kumuhifadhi tu,”amesema Foime

Msemaji wa Takukuru Bw. Musa Misalaba amethibitisha pia Aveva kukamatwa na yupo chini ya ulinzi kwa tuhuma zinazohusu rushwa . Alisema TAKUKURU inafanya kazi kwa misingi ya sheria na yupo katika mikono .

Taarifa ambazo sio rasmi zinaeleza kuwa sababu ya Aveva kushikiliwa na kuhojiwa ni kuhusu zile pesa milioni 450 azilizoingiza katika akaunti yake binafsi akihofia kukatwa kama deni ambalo simba ilikuwa ikidaiwa na TRA. Awali Simba inadaiwa na TRA Milioni 650 ambazo ni sababu ya ukwepaji wa kodi katika Klabu hiyo kongwe.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com