Genk wamzuia Mbwana Samatta kujiunga na kikosi cha Taifa Stars…


KIKOSI cha wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) kinatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Nairobi kwa ajili ya kuwavaa wenyeji Kenya (Harambee Stars) katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayofanyika Jumapili nchini humo.

Mbwana-Samatta-Taifa-Stars-Nahodha-Bongosoka-2

kocha wa Taifa Stars, Boniface Mkwasa alisema kuwa kikosi hicho kilitarajia kuanza mazoezi jana jioni kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo huo unaotambuliwa na kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Mkwasa alisema kuwa kikosi hicho kitamkosa nahodha wake, mshambuliaji Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji kutokana na kubanwa na ratiba ya timu yake.

Mbwana-Samatta-Taifa-Stars-vs--CHAD-AFCON-Bongosoka

“Kuhusiana na Thomas Ulimwengu, bado TP Mazembe hawajatujibu barua yetu ya kumuombea ruhusa tuliyowapelekea, ila leo (jana) tumewakumbusha,” alisema kocha huyo ambaye alifanikiwa kuipeleka Twiga Stars katika fainali za Afrika kwa wanawake zilizofanyika Afrika Kusini 2010.

Aliongeza kuwa kikosi chake kinatarajia kukamilika kwa wachezaji wote wa ndani kuripoti kesho asubuhi baada ya nyota wa Yanga na Azam FC kumaliza kuzitumikia timu zao kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) unaofanyika leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com