Hans pluijm : Mbwana Samatta atacheza ligi ya uingereza


Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm amesema mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kuna uwezekano wa siku moja kucheza katika timu za Ligi Kuu England.

Kauli hiyo ya Pluijm imekuja baada ya nahodha huyo wa Taifa Stars, anayecheza timu ya Genk ya Ubelgiji kufanikiwa kufuzu kucheza nusu fainali ya Europa na timu yake hiyo.

Mbwana-Samatta-Genk-Bongosoka

Pluijm alisema Samatta ni mchezaji wa kuigwa kwa wachezaji wengi wa Tanzania, si kwa uchezaji tu bali hata nidhamu na tabia yake uwanjani na vingine vingi ambavyo vimempa mafanikio na kufikia hapo alipo.

Hans-Pluijm-Yanga

“Samatta ana mbio, ubora, akili, tabia njema na ni mfano mzuri wa kuigwa na wachezaji wengi wa Tanzania kama wanahitaji kufika alipofika Samatta, bado naona mengi mazuri yapo mbele yake kutokana na heshima ya mpira aliyonayo… “Nimesikia pia akihusishwa kuishawishi Manchester United siku ikitokea amekutana nayo kwenye Europa, soka la England siyo kitu chepesi, lakini niseme kwamba kijana Samatta anapambana na mpira una njia zake. “Kiuhalisia mpira hauna mipaka, kama unajitahidi na kuweka nia, utafika popote unapotaka, cha msingi Samatta aongeze bidii zaidi kwa hapo alipofika na atacheza ligi nyingi kubwa,” alisema Pluijm, kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi.

Genk ambayo ilikuwa kundi F imefuzu hatua ya makundi katika michuano ya europa cup baada ya kuifunga  Lokomotiva Zagreb ya Croatia  mabao 4-2 .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com