Hans Pluijm : Yanga hii ni zaidi ya Simba


Wakati uongozi wa Yanga ukisema kwamba benchi la ufundi limekataa kuipeleka timu hiyo Zanzibar kuweka kambi, kocha wa timu hiyo Mholanzi, Hans van der Pluijm, amesema ana kikosi bora zaidi ya wapinzani wake wote katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara. Pluijm, alisema kwamba anakiamini kikosi chake ambacho kimeimarika na hiyo imetokana na kukamilisha programu yake ya mazoezi ya kujiandaa na ligi hiyo kama alivyoiandaa. Pluijm alisema kwamba Yanga ambao ndiyo mabingwa wa Bara, pia wana nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) ambayo watashiriki mwakani.

 Hans-Pluijm--kocha-yanaga-bongosoka
“Tuko tayari, timu yangu imefanya maandalizi mazuri, tumejiandaa kuhakikisha tunashinda mechi za ligi na tutapambana katika mashindano ya kimataifa,” alisema Pluijm. Kocha huyo aliongeza kwamba ushindi wa mechi za mapema utasaidia kupunguza presha kwenye mashindano ya kimataifa na anataka kikosi chake kifanye vizuri na si kutolewa mapema. “Mashindano ya Kombe la Kagame na mechi za kirafiki tulizocheza zimetusaidia kukiimarisha kikosi kwa kuboresha sehemu zilizokuwa na upungufu, kila siku ni siku ya kujikosoa ili kujiimarisha, hakuna kingine zaidi ya kujifunza na kukumbushana,” aliongeza. Naye Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, alisema  kwamba timu yao haitaenda tena Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya mwisho kabla ya kurejea jijini kusubiri kipenga cha ligi. Tiboroha alisema kwamba maamuzi hayo yametokana na kutaka kuwapa nafasi ya kupumzika wachezaji wao ambao baadhi yao watakuwa wamerejea nchini wakitokea kwenye kambi za timu ya Taifa. Yanga itaanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa kuikaribisha Coastal Union Septemba 12 kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam, wakati watani wao wataanzia Tanga kwa kuvaana na African

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com