Harmonize aikomboa Ndanda FC


Baada ya wachezaji wa Ndanda FC kuzuiwa kuondoka katika Hotel ya City Garden mjini Singida kwa kushindwa kulipa Sh 3milioni , Msanii maarufu wa muziki wa BongoFlava , Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize ameweza kuokoa jahazi leo baada ya kutoa kiasi cha shilingi milioni 3.5 .

Ndanda ilikuwa mkoani Singida kucheza mechi ya Ligi Kuu mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Singida United na kuambulia kipigo cha mabao 3-0.

“Kwa niaba ya Ndanda SC tunamshukuru sana @harmonize_tz kwa Msaada wake wa kutupatia Sh Milioni 3 Na Laki 5 (3500000/)ambazo zitasaidia Timu kulipa Deni la Malazi hapa Singida Na kusafiri kesho kurudi Mtwara. Mwenyezi Mungu amjaalie kwenye majukumu yake ya Kila Siku. @babutale  @diamondplatnumz ” Uliandika ukurasa wa instagram wa Ndanda FC .

 

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com