Hatimaye Manchester United Yamuachilia Lukaku


Klabu ya Manchester United hatimaye imekubali kumuachia Mshambuliaji wake Raia wa Ubelgiji , Romelu Lukaku kujiunga na klabu ya Inter Milan ya Italia .

Lukaku mwenye umri wa miaka 26 , anategemea kuwasili nchini Italia muda si mrefu kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi wa afya yake na vipimo .

Uhamisho wa Lukaku unakuja siku chache baada ya nyota huyu kuamua kufanya mazoezi na klabu yake ya zamani ya Anderlecht nchini ubelgiji .

Offer za inter Milan za kumsajili Lukaku zimekuwa zikikataliwa na Mashetani wekundu wa Manchester huku wakiendelea kuongeza offer hadi walipoafikiana .

Manchester United watapata paundi milioni 65 ya papo hapo ikifuatiwa na paundi milioni 12 hapo baadae .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com