Hii ndio timu mpya atakayoichezea Mbwana Samatta huko ulaya…


MENEJA wa mshambuliaji nyota wa TP Mazembe Mbwana Samatta, Jamal Kisongo amesema taratibu za Samatta kujiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji zimekamilika.

Kisongo amethibitisha kila kitu kimeshakamilika na Samata amesaini mkataba wa miaka miwili ambao atakuwa na ridhaa ya kusaini tena mkataba wa miaka miwili baada ya ule wa mwanzo kwisha na kinachosubiriwa ni Samatta kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Ubelgiji maarufu kama Belgian Pro League.

“Mkataba wake na TP Mazembe unamalizika Aprili 30, mwakani hivyo kwa mujibu wa kanuni za FIFA ana haki ya kusaini au kuchagua wapi anataka kwenda na kufanya maamuzi, kwani kanuni ya FIFA, inasema mkataba ukibaki miezi sita na chini ya hapo una haki ya kusaini makubaliano ya awali na hicho ndicho alichokifanya Samatta kwa Genk,” alisema Kisongo.Mbwana-Samatta-TP-Mazembe-Kombe-la-Dunia-la-Vilabu-Bongosoka

 

Kisongo alisema kutokana na hilo ametumia nafasi hiyo kuzungumza na mawakala mbalimbali na mmiliki wa TP Mazembe, Moize Katumbi kuafikiana Samatta aende kucheza Ulaya.

“Ukiondoa Januari, mkataba wake umebaki miezi mitatu ndani ya TP Mazembe miezi hii ndiyo timu ya Genk inaweza kujadiliana na Katumbi kuafikiana watamuachia vipi Samatta kama ni bure majira ya joto au aondoke kwa ada watakayokubaliana,” alisema Kisongo.

Pia Kisongo alisema kwa vile Samatta anakua kisoka, wanaweza kumwona mzuri lakini anaingia katika dunia nyingine ya mpira wa soka, ndio maana wamekubali aende kwenye timu yenye fursa ya kucheza kuliko kwenda moja kwa moja kwenye timu za Ulaya.

“Kulikuwa na timu kadhaa, lakini tuna sababu za kimsingi kwani pamoja na mawakala wetu tulijadiliana tukaona kwamba Genk ni timu muafaka kwa sababu ya ligi yake kwani kumtoa Samatta Afrika na kumpeleka Ulaya moja kwa moja kwenye ligi ngumu itakuwa si kwamba kuonesha ushababi kwamba mtoto anaweza kucheza bali inawezekana tukampoteza na sisi hatutaki kumpoteza tunataka apande ngazi afikie mahali pazuri kwani tunataka apate uzoefu atambue soka la Ulaya likoje,” alisema Kisongo.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com