Ibrahim Ajib aitega Simba…


Mshambuliaji wa klabu ya wekundu wa Msimbazi , Simba , Ibrahim Ajib  ameanza kususia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na kuamua kusubiri hadi  mwishoni wa msimu  ambapo tayari klabu tatu zimeonyesha nia ya kumsajili kama mchezaji huru .

Ajib amegoma kuongeza mkataba Simba SC ili kujirahisishia njia ya kuondoka mwishoni mwa msimu kama mchezaji huru. Habari kutoka ndani ya Simba zimesema kwamba Ajib amegoma kabisa kusaini mkataba mpya Simba SC licha ya kushawishiwa mno kufanya hivyo.

Viongozi wa Simba walitarajia  kua Ajib angeondoka dirisha hili dogo Januari ili wavune dau la uhamisho, lakini kukwama kwa dili hilo ni mwanzo wa mchezaji huyo kuondoka bure Julai mwaka huu.

Ajib alikuwa nchini Misri kwa wiki moja kufanya majaribio katika klabu ya Haras El Hodoud ya Misri ambayo imeripotiwa amefuzu, lakini klabu hiyo ya Alexandria haikutuma maombi yoyote ya kumnunua mchezaji huyo Simba SC.

Simba wana wasiwasi Hodoud wanategea kumsaini Ajib  kama mchezaji huru Julai mwaka huu atakapomaliza mkataba wake.

Lakini wakati huo huo, Hodoud nao wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo nayo inamtaka mchezaji huyo.

Lakini kwa uhamisho wowote, bado Simba inaweza kunufaika kama klabu iliyomlea Ajib – kwani kijana huyo aliibukia timu ya vijana ya klabu hiyo.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com