Je , Mbwana Samatta kuongoza ufungaji bora ligi ya ubelgiji leo ?


Baada ya Jeremy Perbet wa Sporting Charleroi na Sofiane Hanni rai wa Algeria anayekipiga KV Mechelen kuongoza kwa ufungaji bora katika ligi kuu ya ubelgiji maarufu kama Pro League , sasa leo , Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania , Mbwana Samatta leo anatarajia kuanza mbio za kusaka ufungaji bora pale timu yake ya KRC Genk itakapovaana na KV Oostende katika muendelezo wa mechi za ufunguzi katika wa ligi hiyo .

Mbwana-Samatta-Ligi-ya-ubelgiji-Bongosoka

Samatta ambaye aliikutia ligi hiyo mwishoni baada ya kusajiliwa katika dirisha dogo la usajili , Kama atatupia goli mbili kuendelea katika mechi ya leo , basi atakua kajiweka katika nafasi nzuri ya kuanza msimu kwa kuongoza kwa ufungaji kwani katika mechi za jana za ufunguzi hakuna mchezaji hata mmoja aliyeweza kucheka na nyavu zaidi ya mara moja .

Mchezo wa leo utapigwa katika  dimba la Cristal Arena, nyumbani kwa Genk  ambapo utaanza saa 1 kamili za usiku kwa majira ya Tanzania na Afrika Afrika Mashariki kwa ujumla. Msimu uliopita, Samatta aliwafunga Oostende katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi waliyokutana, hivyo kumbukumbu hii ni morali tosha ya kuhakikisha anaisaidia tena timu yake kuibuka na ushindi leo.

Msimu uliopita Genk walimaliza nafasi ya tano baada ya kujikusanyia alama 48 huku Oostende wakimaliza nafasi ya nne baada ya kupata alama 49.

Genk na Oostende wamekutana mara kumi katika michuano tofauti-tofauti. Oostende anaonekana kuwa na rekodi nzuri zaidi baada ya kufanikiwa kushinda michezo 4, huku Genk wakishinda mara 3 na kutoka sare mara tatu.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com