Julio avunja rekodi ya Azam FC, yatoka sare na Mwadui FC…


Mfupa uliomshinda Simba umeendelea kuigomea timu yenye menye meno ya chuma na ukuta wa zege Azam FC, sura tatu zimeonekana kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 na hivyo kutibua Rekodi ya Stewart Hall , Kocha mkuu wa Azam hajawahi kufungwa bao ndani ya dakika 90, yaani alikuwa akishinda au kutoa sare huku akiwa na “Clean Sheet” ndani ya mechi 13.  Winga machachari kipenzi cha Wanamsimbazi, Ramadhan Singano Messi amefungua akaunti ya mabao kwa kuifungia bao pekee Azam FC kwenye sare ya bao 1-1 kabla ya Bakari Kigodeko kuisawazishia Mwadui FC
Kikosi-cha-Azam bongosoka

Kwa ujumla bao la jana la Azam walilofungwa  linakuwa bao la tatu kwa Azam FC kufungwa  ndania ya mechi 15 ilizocheza tangu kurejea kwa kocha Muingereza, Stewart John Hall Juni mwaka huu. Awali ya hapo, ni Friends Rangers pekee walioweza kuupenya ukuta wa Azam FC ya Stewart na kufunga mara mbili wakilala 4-2 katika mchezo wake wa kwanza kabisa wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ni swali ambalo majibu yake yatapatikana mara baada ya msimu mpya kuanza, Julio amekuwa akitamba kunyakua taji la VPL msimu huu, kwa sare mbili dhidi ya vigogo Simba na Azam ingekuwa VPL angekuwa kwenye nafasi nzuri ya kunyakua taji.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com