Kikosi cha Simba kinachoanza leo dhidi ya Ndanda FC…


Pazia  la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2016/17 linatarajiwa kufunguliwa masaa machache yajayo  katika viwanja vitano tofauti hapa nchini huku katika uwanja wa Uhuru, Simba ikiwakaribisha Ndanda FC .

Tayari Simba imeshatoa kikosi chake ambapo habari nzuri kwa mashabiki wa Simba ni kuwepo kwa Laudit Mavugo kwenye kikosi cha wachezaji 11 watakaoanza leo baada ya  kupatikana kwa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) .

LAudit-Mavugo-Simba-Bongosoka

Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema kuwa maandalizi ya timu yake yamekamilika na wachezaji wote wako tayari kuanza mapambano ya kusaka pointi tatu muhimu. Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Ndanda FC leo.

1. Vicent Angban
2. Malika Ndeule
3. Mohamed Hussein
4. Method Mwanjali
5. Juuk Murshid
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Mohamed Ibrahim
9. Laudit Mavugo
10. Ibrahim Ajibu
11-Jamal Mnyate

Wachezaji wa  akiba ni

1. Manyika Peter
2. Hamad Juma
3. Abdi Banda
4. Novaty Lufunga
5. Blagnon Frederick
6. Mussa Ndusha
7. Mzamir Yasin
8. Mwinyi Kazimoto

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com