Kikosi cha Simba mapinduzi cup 2019 kugawanywa kimafia…


Wakati michuano ya mapinduzi cup ikiwa imeshaanza kutimua vumbi hapo Jana , Januari mosi 2019 , Klabu ya wekundu wa Msimbazi ,  Simba tayari imeshawasili visiwani Zanzibar hii leo na kikosi chao kamili cha wachezaji 27 .

Kikosi hicho kinategemewa kugawanywa ifikapo Januari 8 huku wachezaji 19 wakitegemewa kuondoka kuelekea jijini Dar-es-salaam  kuwahi  mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya dhidi ya JS Saoura ya Algeria Januari 12, mwaka huu kwenye  Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam .

Msemaji wa Simba Haji Manara alisema: “Tunatarajia kuondoka Dar kesho (leo) kuelekea Zanzibar na tutashusha kikosi chote kwa kuwa tunatumia nafasi hii kwa ajili ya kujiandaa na mechi za makundi Caf, hivyo ni nafasi nzuri kwetu kujiandaa,” alimaliza.

Simba watashuka katika Uwanja wa Amaan keshokutwa kuivaa Chipukizi ya Pemba.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com