Kikosi cha Yanga mapinduzi cup 2019


Wakati michuano ya Mapinduzi cup ikiendelea kutimua vumbi leo , kifuatacho ni kikosi cha wachezaji 23 wa Yanga kitakachoshiriki michuano hiyo ; –

Kikosi  hicho ni pamoja na Maka Edward, Haji Mwinyi, Said Makapu, Matheo Anthony, Erick Msagati, Deo Mkami, Ibrahim Abrahaman, Ibrahim Ahmed, Deus Kaseke, Mustapha Seleman, Abuu Shaban, Ramadhan Mrisho.

Wengine ni: Mohamed Salumu, Cheda Hussein, Yasini Salehe, Salumu Mkama, Faraji Kilaza, Bakari Athman, Said Khasimu, Shaban Mohamed, Pius Buswita, Juma Abdul na Jaffary Mohamed.

Yanga imetoa mapumziko kwa nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza.

Licha ya kukosekana kwa nyota hao pia Yanga itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Noel Mwandila, kufuatia Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera kurejea kwao DR Congo kwa mapumziko mafupi.

Yanga ambayo ipo kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara kesho itatupa karata yake ya kwanza kwenye Kombe Mapinduzi kwa kuwavaa vinara wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ, mechi inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com