Kikosi kamili cha Simba msimu wa 2018/2019


Wakati zikiwa zimebakia wiki chache msimu mpya wa ligi kuu uanze kutimua vumbi , kikosi cha simba tayari kipo tayari kuianza safari ya kutetea ubingwa wa ligi kuu tanzania bara kwa msimu mpya wa 2018/2019 .

Simba pia  imeweka rekodi ya usajili baada ya  kusajili wachezaji tisa huku usajili wa mshambuliaji wa Gor Mahia, Kagere ukiwa gumzo kwakua watani wao wa Jadi , Yanga nao walikua wakimuwania mchezaji huyo .

Wakati dirisha la usajili likifungwa julai 26 , Simba walifanikiwa kukamilisha usajili wa kiungo Hassan Dilunga pamoja na kumwongeza mkataba kiungo Said Hamis Ndemla na tayari nyota hao wameshatua nchini Uturuki ambako timu hiyo imeweka kambi.

Kikosi kamili ni kama ifuatavyo :-

Makipa:

Aishi Manula, Deogratius Munishi na Ally Salim.

Walinzi:

Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Mohammed Hussein, Nicolas Gyan, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, James Kotei, Yusufu Mlipili, Paul Bukaba, Vicent Costa na Salim Mbonde.

Viungo: Jonas Mkude, Mzamiru Yasin, Shiza Kichuya, Cletus Chama, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga, Mohammed Ibrahim, Marcel Kaheza, Abdul Hamis, Rashid Juma na Said Ndemla.

Washambuliaji:

Emanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Adam Salamba na Mohammed Rashid.

Simba pia itaanza msimu mpya wa ligi kuu na kocha wao mpya raia wa Ubelgiji,  Patrick Aussems, ambaye  ana mkataba wa  mwaka mmoja akiwa anachukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre, ambaye alimaliza muda wake.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com