Kikosi kipya cha Simba utakipenda mwenyewe…


Kwa namna yoyote ile, bila shaka Simba wanahitaji kujenga kikosi kitakachotoa matunda mapema zaidi na hiyo ndiyo sababu inayowafanya viongozi na benchi la ufundi kukisoka kikosi chao kitakachowafikisha kwenye mafanikio ya haraka kwa mwendokasi.

Simba inaimarisha zaidi safu ya kiungo na ushambuliaji ili kuhakikisha wanakuwa na uwezo wa kucheka na nyavu mara kwa mara na kupata ushindi na shughuli inayofanywa na makocha wote huko mkoani Morogoro walikoweka kambi kuwanoa mastraika huku wakihitaji mastraika zaidi.

Kocha Joseph Omog na msaidizi wake, Jackson Mayanja wanachora ramani kujenga kikosi cha kazi , huku shauku yao ikiwa ni kuwa na safu imara ya ushambuliaji ambayo ndiyo imeonekana kuwa tatizo sugu la Simba katika siku za karibuni.

Mastraika hao wanaonolewa kwenye kambi iliyopo kwenye Chuo cha Biblia mjini Morogoro wameanza kurudisha imani ya mashabiki wao kuwa msimu huu, kikosi hicho kitaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Joseph-Omog-na-Jackson-Mayanja-Simba-Kocha-Bongosoka

Washambuliaji waliopo hadi hivi sasa katika kikosi cha Simba ni pamoja na Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib, Danny Lyanga na Blagnon Frederick kutoka Ivory Coast, kwa sasa ndio wanaonekana ndio matumaini mapya ya Simba.

Mbali ya nyota hao kujifua vilivyo kwa ajili ya ushindani, pia nyota wapya kama beki wa kulia, Hamad Juma aliyetokea Coastal Union, Beki wa kati, Method Mwanjali kutoka Zimbabwe na kiungo Mudhamili Yassin anaonekana kufanya vema kwenye mazoezi hayo ya msimu ujao.

Nyota wengine ambao pia hawapo nyuma kwenye ushindani huo wa kukirudisha kikosi hicho kwenye hadhi yake ni Juuko Murshid, Mwinyi Kazimoto, Mohammed Hussein ‘Tshaballa’, Awadh Juma, Peter Mwalyanzi, Said Ndemla, Novat Lufungo, Jamal Mnyate na Haji Ugando.

Kikosi hicho kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya kurudisha hadhi ya klabu hiyo na kuweza kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa  miaka minne kwa sasa.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com