Kocha Simba amtaka haraka pacha wa Kagere…


Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba , imepania kukamilisha usajili wa nahodha wa UD Songo ,  Jose Luis Miquissone , anayecheza kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns iliyopo Ligi Kuu ya Sauzi (PSL).

Kocha mkuu wa Simba , Sven Vandenbroeck, tayari ameuomba uongozi wa klabu hiyo kuharakisha usajili wa mshambuliaji huyo unakamilika haraka .

Licha ya ushindi mnono ambao Simba imekuwa ikiupata chini ya Vandenbrock, lakini Mbelgiji huyo bado amesema haridhishwi na ufanisi wa safu yake ya ushambuliaji,  ambayo inamtegemea zaidi Meddie Kagere na sasa ameuomba uongozi kuharakisha usajili wa Miquissone unakamilika.

 “Kufunga mabao mengi ni silaha kubwa kwa timu,  kazi ya mshambuliaji ni kufunga haijalishi kafunga mabao matano au mangapi, timu yangu inatengeneza nafasi nyingi lakini tumekuwa tukizitumia chache sasa hilo ni tatizo.

“ Nimeuomba uongozi kuharakaisha usajili wa Miquissone, ambaye anaweza kuja kusaidiana na Kagere, lengo langu ni kuzitumia vizuri hizi nafasi tunazotengeneza,” alisema Vandenbroeck.

Inaelezwa kilichoamriwa ni Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa kwenda Afrika Kusini kukamilisha usajili huo .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com