Kuhusu Tegete, Kimwaga na mechi ya Simba na Mwadui


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Jerry Tegete  leo anaweza kua miongoni mwa wachezaji wa mwadui FC watakaoivaa Simba leo baada ya kusaini rasmi mkataba wa miaka miwili kuitumikia Mwadui ya Shinyanga kwa mkataba wa miaka miwili kwenye msimu huu wa Ligi Kuu baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho akiwa mchezaji huru.  Simba leo inaingia uwanjani kukipiga na klabu ya Mwadui FC ya Shinganga mchezo wa kirafiki kujipima ubavu kujiandaa na michuano ya ligi kuu Tanzania bara inayotarajia kuanza mapema mwezi ujao. Timu ya Mwadui FC inafundishwa na kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye amewahi kuicheza klabu ya Simba lakini kadhalika amewahi kuwa kocha wa Simba pia.

Joseph-Kimwaga-Jerry-Tegete-Dylan-Kerr-Julio-mwadui-Simba-bongosoka

Pia katika muendelezo wa kikosi cha Simba ,  kiungo mshambuliaji wake mpya aliesajiliwa kwa mkopo kutoka Azam FC Joseph Kimwaga ameanza rasmi kufanya mazoezi na kikosi cha Simba na leo pia anatajiwa kuonekana uwanjani akifanya yake.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com