Kujituma Simba kwamzawadia gari Mohammed Hussein “Tshabalala”


Mohammed Hussein ‘Tshabalala’  amezawadiwa gari mpya aina ya aina ya Toyota Raum na mwanyekiti wa kamati  ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi za mwanzo wa msimu wa ligi kuu Tanzania Bara .

mohamed-hussein-tshabalala-gari-jipya-simba-bongosoka

Ukiachana na Gari , Tshabalala pia amepewa milioni 1 kwa ajili ya kuliwekea gari lake jipya mafuta kwa kipindi cha miezi 6 . Zawadi hii aliyoipata Tshabalala haikua kwenye mkataba  wake wa sasa unaomalizika mwishoni mwa msimu.

mohammed-hussein-tshabalala-simba
Alipokaririwa na mtandao wa Bin Zubeiry Sports online , Hans Poppe alisema kua anampango wa kutoa zawadi ya aina hiyo kwa mchezaji yeyote mwingine wa Simba SC atakayefuata nyayo za Tshabalala kwa kujituma na kuisaidia timu.
“Hiyo ipo nje ya Mkataba wake, nimempa zawadi tu kutokana na juhudi zake kwa sasa. Na nitatoa zawadi hiyo kwa yeyote ambaye atafuata nyayo zake. Na nadhani zawadi kama hii inanukia kwa Ibrahim Hajib,”alisema Hans Poppe.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com