Laudit Mavugo ana deni kubwa Simba


Mshambuliaji  wa Simba , Laudit Mavugo, ana deni kubwa sana kwenye klabu yake na tayari wekundu wa Msimbazi wameanza  kumkumbusha kuwa hadi kufikia mwisho wa msimu huu mavugo anahitaji kua ametupia mabao 30 baada ya yeye mwenyewe kutoa ahadi hiyo alipokua anasajiliwa akitokea Vital’O ya Burundi .

LAudit-Mavugo-Simba-Bongosoka

 

Licha ya kufunga bao moja katika mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting na kufikisha magoli mawili   katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu, lakini  mavugo alionekana kupoteza nafasi kadhaa za wazi za kucheka na nyavu.

Mavugo alikosa mabao hayo ambayo yangeweza kuipa ushindi mnono zaidi Simba katika dakika ya 26, 29 na 36 kutokana na kukosa umakini pale aliposhindwa kuzitumia pasi mbili za Ibrahim Ajib na moja ya Said Ndemla.

Wakati akisaini mkataba wa kujiunga na Simba, Mavugo alihaidi kufunga  zaidi ya mabao 30 katika msimu huu wa Ligi Kuu ili kuwapa zawadi mashabiki wa Simba ambao wamemsubiri kwa misimu miwili.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com