Laudit Mavugo : Hakuna beki wa kunizuia ligi kuu


Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Simba kutoka Burundi, Laudit Mavugo, amesema haoni mabeki wenye uwezo wa kumsimamisha kasi yake ya kupachika mabao katika mechi za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayo ilianza wiki iliyopita.

Mavugo alisema anafahamu mbinu mbalimbali za kuwatoka mabeki wa timu pinzani ambao wanacheza zaidi soka la kukamia na si kutumia ‘akili’ kwenye kukaba.

Mavugo alisema ushindani kwenye Ligi Kuu ya Tanzania ni mkubwa, lakini uzoefu alioupata katika mechi za kimataifa akiwa na timu ya nchi yake umemsaidia kuwa imara na kumuongezea mbinu za kufunga mabao katika nafasi isiyotarajiwa.

Simba-VS-NDanda-LAudit-MAvugo-Bongosoka

“Timu za Tanzania zinacheza kwa kukamia sana, najua kila mtu ananiangalia mimi, hiyo hainisumbui, nitafanya kila ninaloweza ili kuisaidia timu yangu ipate ushindi katika kila mechi,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Vital’ O.

Aliongeza kuwa anafurahia mazingira ya Tanzania huku akieleza kwamba ‘sapoti’ wanayoipata kutoka kwa mashabiki wa Simba, kwake anafananisha na deni na kutwaa ubingwa wa ligi ndiyo, jambo pekee wanalotakiwa kulitekeleza.

“Ligi ni ngumu, ila ushindi ni muhimu, tunataka kushinda pia mechi inayofuata,” Mavugo alisema kwa kifupi.

Mshambuliaji huyo aliongeza kuwa amekuja nchini kuisaidia Simba ili kutwaa mataji mbalimbali na hakuja kupambana kuvunja rekodi iliyowahi kuwekwa na wachezaji wengine wa kimataifa.

Simba inatarajia kuingia kambini leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya JKT Ruvu utakaofanyika Jumamosi.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com