(Live Updates) Second Half imeanza, Taifa Stars na Uganda The Cranes hakuna aliyeona lango la mwenzake


Mchezo kati ya Taifa Stars na Uganda hivi sasa  kipindi cha pili ndio kimeanza  ambapo magoli bado ni bila bila  ingawa dakika ya 17 ya mchezo Taifa Stars ilipata  goli kutoka kwa John Bocco lakini lilikataliwa kutokana na Bocco tayari kua amekwishaotea baada ya kupokea pasi nzuri ya Rashid Mandawa.  Mchezo ulianza kwa kasi ambapo dakika ya kwanza Taifa Stars waliweza kupata kona ambapo mbio za Simon Msuva kuliona lango la The Cranes zilisitishwa na beki wao , Brian Ochwo . Dakika ya 29 , Farouk Miya wa Uganda alipiga shuti kali la mbali ambalo liliokolewa na kuzaa kona. Vikosi ni kama ifuatavyo :-

Uganda-VS-Taifa-Stars-1

Walioanza Uganda: James Alitho (GK), Denis Okot Oola, Brian Ochwo, Hassan Waswa Mawanda – Capt, Shafiq Bakaki, Derick Tekkwo, Muzamil Mutyaba, Erisa Sekisambu, Farouk Miya, John Semazi, Robert Sentengo.

Walioanza Taifa Stars: Ally Mustafa Mtinge (GK) , Nadir Haroub Ali, John Raphael Bocco, Salum Shomari Kapombe, Frank Domayo Raymond, Saimon HappyGod Msuva, Kelvin Patrick Yondani, Mwinyi Haji Mngwali, Rashid Y. Mandawa, Deus Kaseke David, Abbas Mudathiri Yahya.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com