Mabadiliko Yanga yanukia , Hisa za Bilioni 50 zatengwa…


Mabadiliko anayotaka mfanyabiashara Mohammed Dewji MO kwenye klabu ya Simba yanaonekana kuitia presha Yanga ambayo katika mkutano wa dharura wa Jumamosi, suala la mabadiliko huenda likawa ajenda.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndio yatajadiliwa ambapo klabu inataka  kutoka mfumo wa sasa hadi kuwa mfumo wa hisa ambapo taarifa zinaeleza wazi kwamba kuna tajiri mmoja yuko tayari kununua hisa asilimia 40 kwa shilingi bilioni 50.

mbali na tajiri huyo atakayetoa fedha hizo, pia kuna matajiri wengine ambao wako tayari kununua hisa kwa kiasi kikubwa cha fedha ambapo hadi sasa matajiri walioonesha nia ya kununua hisa wamefikia wanne na hisa ambazo wamepanga kununua ni asilimia 54 kwa pamoja.

Yusuph-Manji-Yanga-Bongosoka

Yanga ndiyo iliyoanza utaratibu huo mwaka 2007, ukaishia hewani kabla ya hivi karibuni MO akitaka amilikishwe asilimia 51 ya hisa za Simba.

Katibu mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alipoulizwa kuhusu mkutano huo hakutaka kuzungumzia akidai haelewi ajenda itakuwa ipi na kuwataka wanachama wajitokeze kwa wingi kwani kila kitu kitajulikana huko.

Wakati huo huo, Yanga imetangaza kiingilio cha Sh 5,000 kwa majukwaa yote kwenye mechi yao ya kirafiki dhidi ya Mtibwa itakayopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com