MAKAPTENI bora zaidi ktk historia ya ligi ya Uingereza…


Ligi ya England imekuwa ni moja kati ya ligi bora na pendwa kutokana na namna ambavyo imekuwa ikifuatiliwa Zaidi na watu wengi ulimwenguni.

Ligi hii imetoa makocha bora, wachezaji bora, timu bora na nyuma ya hayo yote huwa kunakuwepo viongozi bora, nadni ya timu tunawagusia Zaidi manahodha.

Hawa ndio manahodha bora zaidi ambao wamewahi kuongoza timu zinazoshiriki ligi kuu ya England, maarufu kama EPL.

Roy Keane

1. Roy Keane

Roy Keane, alishinda mataji 17 akiwa na Manchester United, ikiwemo ile tatu kubwa ya EPL, FA, na UEFA (Treble) mwaka 1999.

Mechi za ligi:366

Mabao: 39

Klabu : Nottingham Forest, Manchester United

Mataji ya ligi: Saba (7)

John Terry

2. John Terry

John Terry ndiye nahodha mwenye mafanikio zaidi ndani ya Chelsea, akishinda mataji 17, yakiwemo matano ya ligi kuu ya England.

Mechi za ligi: 492

Mabao: 41

Klabu: Chelsea

Mataji ya ligi: Matano (5)

Steven Gerrard

3. Steven Gerrard

Steven Gerrard ni mchezaji pekee kufunga katika fainali 4 tofauti (za FA, Kombe la ligi, Uefa cup na ligi ya mabingwa Ulaya/Champions league)huku akishinda na kutwaa ubingwa katika zote.

Mechi za ligi: 504

Mabao:120

Klabu: Liverpool

Mataji ya ligi: kapa

Tony Adams

4. Tony Adams

Tony Adams ametumia muda wake wote katika soka akiitumikia Arsenal huku akishinda mataji 13 katika kipindi cha mwaka 1983 mpaka 2002

Mechi za ligi: 255

Mabao: 12

Klabu: Arsenal

Mataji ya ligi: Mawili (2)

Patrick Vieira

5. Patrick Vieira

Patrick Vieira ndiye aliyeiongoza Arsensl katika msimu wao ambao walitwaa ubingwa wa ligi ya England, bila kupoteza mchezo hata mmoja (Invicibles) 2003-04.

Mechi za ligi: 307

Mabao: 31

Klabu:Arsenal, Manchester City

Mataji ya ligi: Matatu (3)

Vincent Kompany

6. Vincent Kompany

Vincent Kompany aliondoka  Manchester City mwezi Mei, 2019 baada ya misimu 11 ya mafanikio ndani ya dimba la Etihad.

Mechi za ligi: 265

Mabao: 18

Klabu: Manchester City

Mataji ya ligi: Manne (4)

7. Nemanja Vidic

Nemanja Vidic ameshinda mataji matano (5) ya ligi akiwa kama nahodha wa Manchester United, mawili (2) kati ya hayo ameyatwaa akiwa kama nahodha.

Mechi za ligi: 211

Mabao: 15

Klabu: Manchester United

Mataji ya ligi: Matano (5)

Allan Shearer

8. Alan Shearer

Alan Shearer anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya England kwa muda wote katika historia ya ligi hiyo akiwa na mabao 260 katika mechi 441.

Mechi za ligi: 441

Mabao: 260

Klabu: Blackburn, Newcastle

Mataji ya ligi: Moja (1)

Jordan Henderson

9. Jordan Henderson

Jordan Henderson ameiongoza Liverpool kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya, Uefa super cup na kombe la klabu bingwa dunia mwaka 2019 lakini bado hajawahi kutwaa taji la ligi.

Mechi za ligi: 335

Mabao: 29

Klabu: Sunderland, Liverpool

Mataji ya ligi: Kapa – japo Liverpool wanaongoza kwa alama nyingi zaidi na uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu wa 2019-20.

Wes Morgan (Kapteni Morgan)

10. Wes Morgan

Wes Morgan alikuwa ni mchezaji wa tatu kwa wachezaji wa ndani kucheza kila dakika (dakika zote) katika mechi zote za msimu ambao timu yake imetwaa ubingwa, 2015-16.

Mechi za ligi: 164

Mabao: 8

Klabu: Leicester

Mataji ya ligi: Moja (1).                                                                                         

Vipi kwa upande wako, unahisi nani ni nahodha bora zaidi ? , tuandikie kwenye comment hapa chini.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com