Mamilioni ya Okwi yatua Simba


Klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark imelipa fedha za uamisho wa Okwi ambaye alijiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa mwezi Julai.Klabu ya Simba  yenye makao yake mtaa wa msimbazi imepokea fedha kiasi cha   Sh milioni 220 kuingia katika akaunti yao. Fedha hizo ni malipo ya mauzo ya mshambuliaji Emmanuel Okwi Arnold kwenda katika klabu ya Sonderjyske ya nchini nchini Denmark. Sonderjyske ilikubali kulipa dola 110,000 ili kumnasa Okwi. Ikaahidi kulipa fedha hizo Juni 17 na imechelewa kidogo tu lakini imeweza kutimiza ilichoahidi. Habari za uhakika kutoka Simba, zimeeleza kuwa Sonderjyske imeilipa Simba kupitia akaunti yake ya CRDB jijini Dar es Salaam.

Hans-Poppe-okwi--usajili--bongosoka

Tayari Okwi yuko nchini Denmark katika kikosi chake cha Sonderjyske akiendelea kuitumikia timu yake. Kama ilivyoelezwa na uongozi wa Simba kwenye taarifa ya awali juu ya Uamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi, fedha hizo zitatumika kwenye usajili na kuimarisha nguvu kwenye kikosi cha Simba.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com