Manchester United kumuachia Pogba kwa sharti hili


Klabu ya Manchester United imeiambia Inter Milan kwamba kama inataka kumsajili Paul Pogba basi lazima mshambuliaji wao Lautaro Martinez atue Old Trafford.

..

Pogba ambaye kwasasa hajatulia United anatarajiwa kuungana na kocha wake wa Zamani , Antonio Conte .

Martinez ana thamani ya paundi milioni 80 huku Manchester united ikisisitiza kua Pogba thamani yake ni paundi milioni 150.

Pamoja na tabiri nyingi kua Pogba ataondoka kipindi hiki cha usajili , bosi wa Old Trafford , Ole Gunnar Solskjaer’s amesemekana bado kumuhitaji .

Kwa upande wa Pogba , tayari aliweka bayana kua anaona siku za usoni akiwa nje ya Old Trafford huku akihusishwa na kuamia moja ya timu kubwa ulaya .

Kwasasa Pogba yupo nje kwa wiki kadhaa akiuguza jeraha la kifundo cha mguu .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com