Mapinduzi Cup kuanza kupamba moto leo…


Wakati michuano ya Mapinduzi cup ikianza hapo Jana , Januari mosi , leo kutakua na mechi mbili ambapo mchezo wa kwanza wa saa 10:00 jioni, Chipukizi wataikaribisha Mlandege na mchezo wa saa 2:00 usiku, Azam FC itawakaribisha Jamhuri SC. Mechi zote zitapigwa katika uwanja wa Amaan.

Michuano hii hufanyika kila mwanzoni mwa mwaka kuanzia Januari mosi hadi kilele cha sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12.

Katika mchezo wa ufunguzi ,  KVZ SC walitoa sare ya bila kufungana na Malindi SC .

Kumbuka michuano ya Mapinduzi Cup  mwaka huu inashirikisha jumla ya timu 9, baada ya URA ya Uganda na Bandari ya Kenya kunyimwa ruhusa na mashirikisho yao ya soka kuja kushiriki michuano hiyo.

Kwa upande wa Tanzania bara safari hii unawakilishwa na timu tatu pekee tofauti na mwaka jana zilikuwa timu nne, timu ambazo zinaiwakilisha Tanzania bara katika michuano hiyo ni Simba SC, Azam FC ambao ndio Mabingwa watetezi na Yanga SC.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com