MARC-Vivien Foe na Jezi ya heshima Man City…


Marc-Vivien Foe wa Manchester City akipambana na mchezaji wa Manchester United, Juan Veron mwaka 2002.

Dunia inakumbuka huyu mwamba kwa ukabaji wake wakutumia nguvu na akilili, umbo lake lenye misuli mingi iliwapa taabu viungo wengi kuchukua mpira kwenye miguu yake.

Marc Vivien foe alizaliwa may 1 1975 huko yoaunde Cameron, na kuanza kucheza soka akiwa na umri wa miaka 16 kwenye academy ya union de garoua huko nyumban kwao yoaunde.

Foe alizaliwa kwenye kizazi cha zahabu cha Cameron kilicho shinda kombe la mataifa ya Africa mara mbili mfululizo 2000 na 2002.
Kikosi kilichoundwa na nyota kazaa Kama Patrick Mboma, Samuel etoo, Rigobet song, Pierre njaka, foe mwenye na nyota wengine kibao.

Marc-Vivien Foe na Nicolas Anelka ndani ya Manchester City.

Je ushawai kujiuliza kwanin kwanini club ya Manchester city jez no 23 haitumiki. Yaan hakuna mchezaj anaeivaa jezi hiyo au kujiuliza mwaka 2017 timu ya taifa ya Cameron ilipo ifunga timu ya taifa ya Egypt kwenye mchezo wa final wa mataifa ya Africa afcon.

Jezi no 17 ilionekana Sana kwenye mchezo ule mashabiki wa Cameron walikua wameivaa kwa wingi na ubingwa ule wa afcon ulikua dedication kwa kwa jezi hiyo.

Foe alianza maisha ya soka la kulipwa kwenye club ya lens huko ufaransa mwaka 1994- 1999 . Baadae alitimukia ligi kuu ya England kwenye club ya West Ham mwaka 1999 mpaka 2000.

Mwaka 2000 alijiunga na club ya Lyon ya ufaransa mpaka mwaka 2002.Mwaka 2002 alijiunga Manchester City kwa mkopo ambayo aliitumikia mpaka mauti yana mfika.

Mwaka 2003 ndio ulikua mwaka mbaaya kwa mashabiki wa soka kote ulimwengu, na ulikua mwaka wa mwisho kwa huyu shujaa wa Africa kuvuta pumzi hapa dunian.
Dunia ilijawa na huzuni hususani mashabiki wa soka kote dunian kwan walimshuhudia foe akiangaika kupambania uhai wake pale ufaransa.

Katika michezo huo foe alionekana kuchoka Sana na kocha alipotaka amfanyie mabadiriko foe alitoa uishara Bado kua anataka kuendelea kucheza, kama angejua nin kingetokea bhas angekubali kutolewa la kini kifo hakizuiliki.

Dk ya 72 mchezo foe alianguka katikati ya uwanja ambapo hakukua na mchezaj yeyote karibu yake , foe alikua anahangaika kuokoa maisha yake.Tatizo la moyo ndio lililo muua foe. Foe alitolewa uwanjan akiwa Hana fahamu, alifikishwa kwenye kituo cha kutolea huduma ya kwanza cha uwanja na Alifariki mda mfupi baada ya kufikishwa kituon hapo.

Foe aliwatoa machoz mashabiki wengi wasoka walio kusanyika kuangalia mchezo ule pale Lyon ufaransa.

Mchezaj wa ufaransa Thierry Henry alilia kwa uchungu Sana kwenye mchezo Kati ya ufaransa na Cameron.

Foe aliacha alama kwenye mchezo wa soka ni pale tu shirikisho la mpira la Cameron walipo tangaza kutoitumia jezi no 17 ambayo ilikua inavaliwa na Marc vien Foe..

Mwaka 2003 meneja wa Manchester city kwa wakati ule Kelvin Keegan alitangaza kutotumika tena jez no 23 ilikua inavaliwa na Marc Vivien foe alifanya hivyo ili kumuenzi foe. Ikumbukwe mpaka anakufa alikua mchezaj wa Manchester city.

Mwaka 2017 Cameroon ilipo shinda taji la afcon walilifanya kama zawadi kwa Foe.

By @officialtimothyjr

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com