Matokeo mechi ya Yanga vs Tanzania Prisons


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara , YANGA SC imeendelea kung’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 3-0 Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. atika mchezo wa leo yanga SC walianza kupata goli kupitia kwa Mbuyu Twite aliyemalizia mpira alio utema kipa wa Prisons Mohamed Yusuf katika dakika ya 30. Wakati timu zinajiandaa kwenda mapumziko Amisi Tambwe aliiandikia yanga goli la pili katika dakika za nyongeza na kuipeleka yanga mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Yanga-vs-Tanzania-prisons-matokeo-bongosoka
Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi, huku Prisons wakisaka goli, wakati yanga wakisakata soka safi na kusaka goli lazidi ndipo katika dakika ya 59 yanga walipata penati iliyopigwa kwa ufasaha na Donald Ngoma na kuipa yanga ushindi wa goli 3-0. Yanga SC wamefikisha pointi 6 wakiwa na magoli 5 ya kufunga huku wakiwa bado hawajaruhusu goli katika nyavu zake na kujikuta wakiwa kileleni mwa ligi.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com