Matokeo Simba VS Ndanda FC ..


Mabingwa wa kombe la mapinduzi Simba SC wameuanza vyema mwaka 2016 kwa ushindi wa goli moja bila mbele ya Ndanda FC na kupanda mpaka nafasi ya 3 wakiishusha mtibwa sugar hadi nafasi ya 4.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Nangwanda sijaona uliaribiwa na ubovu wa uwanja na kupelekea kipindi cha kwanza kutumika mipira mirefu zaidi huku wachezaji wakiteleza kutokana na mvua iliyonywesha asubuhi ya leo katika mkoa wa Mtwara.

Ibrahim-HAJIBB--Simba-Bongosoka


Simba SC walipata kona zaidi ya saba katika kipindi cha kwanza lakini wakishindwa kuzitumia, huku Ndanda Fc wakifika langoni mwa Simba SC mara 5.

Kipindi cha pili Simba SC walianza kwa mabadiliko ya kumpumzisha Kiongera na kuingia Ibrahim Ajibu mabadiliko yaliyo wapa utawala wa mchezo simba SC na kuanza kucheza soka la kuonekana japo uwanja ulikuwa hauruhusu.

Katika dakika ya 62 Kocha Kerr alimpumzisha Brian Majegwa na kumuingiza Said Khamisi Ndemla na kuplekea kuongeza kwa kasi ya ushambuliaji ya Simba SC.

Krosi ya Danny Lyanga katika dakika ya 80 na kumkuta Hamisi Kiiza ambapo shuti lake liligonga mwamba na kumuta Ibrahim Ajibu na kuipatia Simba SC goli pekee la ushindi katika mchezo wa leo.

kuingia kwa goli hilo kuliongeza umakini kwa Simba SC na kupelekea mchezo kumalizika kwa simba sc kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kushika nafasi ya 3.

 

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM BAADA YA MCHEZO WA LEO

RnTimuPWDLFAGdPts
1Azam FC1311202781935
2YANGA1310303052533
3SIMBA SC138322091127
4MTIBWA SUGAR13832178927
5MWADUI FC136431612422
6STAND UNITED137151411322
7T. PRISONS136341314-121
8TOTO AFRICANS134541215-317
9MGAMBO SHOOTING13346713-613
10JKT RUVU133371520-512
11MBEYA CITY132561115-411
12MAJIMAJI FC13328823-1511
13NDANDA FC13166915-69
14Coastal Union13166614-89
15KAGERA SUGAR13238416-129
16AFRICAN SPORT132110314-117

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com