Matokeo Simba VS Yanga , Yanga yailamba simba 2 – 0….


Dakika 90 za Mchezo wa ligi kuu Vodacom kati ya Simba SC na Yanga FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salamaa zimemalizika kwa timu ya Yanga kuibamiza Simba SC Bao 2-0 katika mechi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu  Tanzania Bara .

Katika mchezo wa leo ,  Simba SC  walicheza pungufu kwa takribani dakika 66  baada ya beki wake Abdi Banda kuzawadiwa kadi nyekundu katika dsakika ya 23 ya mchezo ikiwa ni baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Abdi-Banda-Simba-Kadi-Nyekundu

Yanga sc waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika ya kwanza kama mpigaji wa faulo angeipiga vyema yanga wangeandika goli la kwanza lakini mpira wake uliishia mikononi mwa kipa Vicent Agban.

Baada ya kosa kosa hiyo Simba SC nao walijibu pigo na kuendelea kushambuliana kwa zamu kwa dakika 23 za mwanzo kabla ya Banda kupewa kadi nyekundu.

Yanga SC waliandika goli la kwanza katika dakika ya 39 kupitia kwa Donald Ngoma ambaye aliwahi mpira ambao Hassan Kessi aliurejesha kwa kipa na mpira kuwa mfupi na kupelekea Ngoma kumchambua kipa na kuiandikia Yanga goli la uongozi.

Donald-Ngoma-Simba-vs-Yanga-Bongosoka

Goli hilo lilpeleka Yanga kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, na katika kipindi cha pili Simba SC walijaribu kusaka goli la kusawazisha bila mafanikio.

Katika dakika ya 71 Amisi Tambwe akiungfa krosi ya mtokea benchi Geofrey Mwashiuya na kuiandikia yanga goli la pili, goli lililo imaliza Simba SC na kupelekea kupoteza mchezo kwa kukubali kufungwa goli 2-0 na yanga.

Ushindi huo wa pili msimu huu Yanga SC wanaupata mbele ya Simba SC unaifanya Simba SC kushuka mpaka nafasi ya tatu huku Yanga ikirejea kilelelni na Azam FC wakishika nafasi ya pili.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com