MAtokeo VPL , Simba Yaipiga Mtibwa sugar goli 1 – 0


Kocha kutoka Uganda wa Simba SC Jackson Mayanja ameeanza kibarua chake kwa ushindi mbele ya Mtibwa sugar ambao ndio walikuwa wa mwisho kukabiliana na kikosi cha simba sc chini ya kocha Kerr ambaye alitimuliwa baada ya kupata kichapo toka kwa timu hiyo.

Katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Simba SC waliibuka na ushinidi wa goli 1-0 mbele ya wakata miwa hao wa Morogoro.

Amissi-Kiiza-Simba-goli-bongosoka

Simba Sc walianza mchezo kwa kasi huku Mtibwa wakiwa chini na katika dakika ya 5 Hamisi Kiiza aliipatia SImba SC goli la kuongoza akimalizia krosi ya Mohemmed Hussein Tshabalala.

Kuingia kwa goli hilo kulizidisha utawala kwa simba sc na katika dakika ya 25 ndipo Mtibwa sugar walianza kuweka mpira katika himaya yao  lakini wakishindwa kutumia nafasi chache walizotengeneza.

Katika kipindi cha pili Mtibwa sugar walijaribu kutenegeneza nafasi kadhaa lakini walishindwa kuzitumia na kupelekea mchezo kumalizika kwa simba sc kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani ulimalizika kwa Coastal union kutoka sare ya goli 1-1 na Majimaji ya Songea, magoli yakifungwa na Dany Mrwanda na Abasalim Chedebel.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com