Matokeo ya APR VS AL SHANDY Kagame Cup


Pamoja na kikosi cha APR ya Rwanda kuondokewa na mlinzi wake mahiri , pin Emery Bayisenge aliyeenda kukipiga klabu ya  Lask Linz FC ya nchini Austria, Kikosi hicho leo kimeondoka na usindi mfinyu wa goli 1 – 0   dhidi ya Al Shandy  ya Sudan.  Katika mchezo huo wa fungua dimba la mashindano haya yanayoshirikisha klabu kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa saa 8 mchana , goli pekee la APR lilifugwa kipindi cha pili  na Bizimana Djihad  lilitosha kuwapa APR Ushindi. Kwasasa APR wanaongoza Kundi B huku wakisubiri mechi nyingine baina ya LLB AFC ya Burundi dhidi ya Heegan ya Somalia.

APR--Al-Shandy-CECAFA-Kagame-Cup

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com