Matokeo ya Mechi ya Taifa Stars na Uganda , Taifa Stars yafungishwa virago CHAN


Taifa Stars, leo imefungishwa rasmi virago katika mbio za  kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kutoka suluhu ya goli 1 –  1   na Uganda the Cranes na hivyo kuweka jumla ya mabao  4 kwa Uganda na 1 kwa Tanzania kutokana na kufugwa goli 3 bila majibu katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Karume, Zanzibar. Katikaa mchezo huo wa marudiano Taifa Stars ilipata  goli  dakika ya 17 ya mchezo kutoka kwa John Bocco lakini lilikataliwa kutokana na Bocco tayari kua amekwishaotea baada ya kupokea pasi nzuri ya Rashid Mandawa .

Uganda-VS-Taifa-Stars-2
Goli la Stars liliwekwa kambani na John Bocco kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Uganda kunawa mpira akiwa kwenye eneo hatari na mwamuzi wa mchezo kuamuru ipigwe penati.  Uganda walisawazisha goli hilo dakika chache baadae kupitia kwa Robert Sentongo baada ya mabeki wa Stars kutegeana kuondosha mpira kwenye eneo la hatari na kufanya matokeo kuwa 1-1. Ramadhani Singano ‘Messi’ aliingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva wakati Said Ndemla aliingia kuchukua nafasi ya Frank Domayo na Rashid Mandawa akapumzishwa kumpisha Salumu Telela.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com