Matokeo ya Simba vs Mwadui , Kipa azimia Uwanjani…


Klabu ya wekundu wa Msimbazi , Simba leo jioni wametoka sare ya bila kufungana na Mabingwa wa ligi daraja la kwanza , Mwadui FC  ya shinyanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Taifa leo jioni. Simba ikichezesha nyota wake wote wapya isipokuwa wale waliopo kwenye  kikosi cha Taifa , Taifa Stars kilichopo Uturuki  imejikuta ikishindwa kuonesha makali yake mbele ya Mwadui FC . Katika tukio la kusikitisha , golikipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, Shaaban Hassan Kado wa Mwadui FC ya Shinyanga amekimbizwa hospitali baada ya kuzimia  dakika ya 77 baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wakati wa purukushani kwenye lango la Mwadui na nafasi yake ikachukuliwa na Jackson Abdulrahman.

Simba-SC-vs-Mwadui-FC-mchezo-wa-kirafiki-uwanja-wa-taifa-bongosoka--matokeo

Katika mchezo wa leo Simba SC walikuwa wanampima mshambuliaji wao toka Senegal Niang huku wakimtumia kwa mara ya kwanza mchezaji wao mpya walio mchukuwa toka Azam FC kwa mkopo Joseph Kimwaga. Simba SC walitengeneza nafasi kadhaa za kujipatia goli lakini waliishia kupoteza nafasi hizo, sambamba na Mwadui ambao walitengeneza nafasi chache na kushindwa kuzitumia nafasi hizo. Kikosi cha Mwadui kinachonolewa na kocha Jamhuri Kihwelo Julio, kimekuwa kikosi cha kwanza kuambulia sare kwa Simba SC inayonolewa na Muingereza Kerr. Kabla ya Mchezo wa leo kikosi cha Kerr kilikuwa bado hakijaambulia sare wala kufungwa katika michezo aliyo kiongoza huku leo akiambulia sare ya kwanza dhidi ya kikosi kinachoundwa na wachezaji wengi walio wahi kutamba na Simba SC na Yanga. Mshambuliaji wa zamani wa yanga Jerry Tegete aliichezea leo Mwadui mchezo wa pili toka ajiunge na timu hiyo yenye maskani yake mkoani Shinyanga.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com