Matokeo ya Taifa Stars na Uganda haya hapa….


Licha ya RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwaahidi shilingi millioni 21  yaani milioni 1 kwa kila mchezaji kama wakiwafunga Uganda, timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba nyumbani  baada   ya kufugwa goli 3 bia majibu na Uganda na kufanya safari yao ya kuelekea kwenye fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaochezea timu za ndani kua ngumu.   Ili isonge mbele, Stars italazimika kushinda 4-0 katika mchezo wa marudiano huko Uganda, jambo ambalo kimahesabu ni gumu sana kutokea hususan kutokana na soka bovu la Taifa Stars.

Kikosi-cha-Taifa-Stars

Mpira ulianza wachezaji wa timu zote mbili kucheza mpira wa kubutuabutua lakini baada ya dakika kadhaa mpira ulitulia na timu zote kuanza kupanga mashambulizi. Lakini Stars bado wameendelea kuwa na matatizo yaleyale ya kupoteza nafasi zinazopaikana kwa kukosa umakini pindi wanapokuwa kwenye eneo la hatari la timu pinzani. Goli la kuongoza la Uganda lilifugwa na mshambuliaji wao, , Erisa Ssekisambu katika dakika ya 39 ya mchezo. Dakika ya 63 Erisa Ssekisambu aliwaongezea Uganda bao la pili huku  goli la 3 likifugwa kwa mkwaju wa penalti na Farouk Milya dakika ya 88. Hadi mchezo unaisha matokeo yakawa 3 bila majibu na kuwaacha mashabiki akishikwa na hasira hadi kocha wa Taifa stars ,Mart Nooij ikabidi asindikizwe nje ya uwanja na ulinzi mkali wa polisi kutokana na kuogopa kupigwa na mashabiki wenye hasira kali.

 NOOIJ asindikizwa na  POLISI

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyekuwa mgeni rasmi wa pambano hilo, alishuhudia Taifa Stars ikishindwa kutengeneza nafasi za kufunga huku ikicheza soka la kujilinda zaidi. Kwa upande wa Stars, kocha wake Mart Noolj amesema anajiskia vibaya na kila mtu anajisikia vibaya kwa matokeo yaliyopatikana. “Tumepoteza nafasi kadhaa na baadae tukaruhusu magoli, nimeumizwa sana lakini hakuna la kufanya zaidi ya kujipanga kwa mchezo wa marudiano,” alisema kocha huyo ambaye alipewa mechi tatu ili kuokoa kibarua chake. Mart Noolj alitolewa uwanjani kwa ulinzi mkali wa polisi ili kumnusuru na mashabiki wenye hasira.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com