Matokeo ya Yanga na SC Villa Haya hapa na yote kuhusu mechi hiyo…..


Mabigwa  wa soka Tanzania bara, Young Africans wametoka suluhu  ya bila kufungana na SC Villa ya Uganda ‘Jogoo’ katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyomalizika usiku huu uwanja wa Taifa Dar es salaam. Hata hivyo, Yanga wangeibuka kidedea, lakini katika dakika ya 79′ winga wake hatari Saimon Msuva alikosa mkwaju wa penalti uliotokana na kiungo mshambuliaji mpya wa Jangwani, Deus Kaseke baada ya  kuangushwa na mlinda mlango wa Villa.

Kikosi-cha-Yanga-Vs-SC-Villa

Mechi hii ya Hisani ya kuchangia ujenzi wa kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu hususani wenye ulemavu wa ngozi, Albino, ilichelewa kuanza kwa zaidi ya saa moja kwasababu Villa hawakufika uwanjani kwa kile kilichoelezwa kwamba waligoma kutokana na kutolipwa fedha na waandaji wa mechi. Yanga imewatumia wachezaji wake wapya, Geofrey Mwakiuya, Malimi Busungu na Deus Kaseke, lakini haikuweza kufua dafu mbele ya Jogoo.Kingine kilichowaacha mashabiki mdomo wazi ni kuonekana kwa Lansana Kamara  akiichezea SC Villa huku ikiwa ni siku chache tu baada ya kutoswa Yanga kwa kutokuonyesha kiwango cha kuridhisha. Mechi ya leo imekua ni kama kipimo cha kuona kama wataweza kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame yanayotarajiwa kuanza mapema mwezi julai.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com