Matokeo ya Yanga VS Azam FC


Uimara wa kucheza penati wa kipa wa Azam FC Aishi Salum Manula umeiokoa Azam FC kupokea kichapo cha kwanza katika msimu huu wa ligi kuu ya vodacom baada ya kulazimisha sare ya goil 1-1 dhidi ya yanga mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo wa leo ambao kila timu ilijaza viungo wengi na kupelekea kukosekana utulivu katika eneo la kati ya uwanja katika kipindi cha kwanza, na kuonekana mchezo kuwa sawa kwa pande zote mbili. Azam FC ndio walikuwa wa mwanzo kufika langoni mwa yanga lakini krosi ya Faridi Mussa Maliki ilikosa mmaliziaji na kupelekea walinzi wa yanga kuokoa hatari hiyo.  Baada ya Azam kupoteza nafasi hiyo nayo Yanga ilitengeneza nafsi mbilia kupitia kwa Kelvin Yondani na Donald Ngoma.

Yanga-SC-VS-Azam-FC-matokeo-bongosoka

Katika dakika ya 45 Donald Ngoma aliimalizia vyema krosi ya Juma Abduli na kuipeleka yanga waende mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0. Kipindi cha pili Yanga walirejea kwa kasi na kujaribu kutengeneza nafasi kadhaa ambazo walishindwa kuzitumia kabla ya Stewart Hall kuurejesha mchezo kuwa sawa pale alipompumzisha Kipre bolue na nafsi yake kuchukuliwa na Franky Domayo.

Katika dakika ya 82 mtyokea benchi Kipre Hermana Tcheche aliisawzishia Azam FC goli, akimalizia pasi safi ya Faridi Mussa Maliki. Dakika mbili mbele yanga walipata penati ambapo Thaban Kamusoko aliipoteza penati hiyo baada ya kipa Aishi Salum Manula kuichezeza penati hiyo iliyo leta tafrani. Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa Yanga walikuwa wanagoli 1 na Azam FC pia wakiwa na goli 1. Katika uwanja wa Nangwanda sijaon Ndanda FC wao wamelazimishwa sare na Toto African ya Mwanza, ya bila ya magoli, huku Atupele Green wa Ndanda FC akipoteza penati katika kipindi cha pili.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com