Matokeo Yanga VS TP MAzembe : Yanga yachapwa 1 – 0 …


Wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, Yanga  imecheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya TP Mazembe ya Congo DRC na kukubali kichapo cha goli 1 – 0 .

Yanga ambayo ilifanya maandalizi kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuweka kambi Uturuki na kuwaruhusu mashabiki wa soka nchini kutizama mchezo huo bure katika uwanja wa Taifa, ilianza mchezo huo dhidi ya TP Mazembe kwa kasi lakini ilishindwa kutumia vyema nafasi zilizotengenezwa.

Yanga-VS-TP-MAzembe-DOnald-Ngoma

Kipindi cha pili TP Mazembe walionekana kubadilika na kuanza kufanya mashambilizi machache katika lango la Yanga na katika dakika ya 75 walifanikiwa kupata goli kupitia mchezaji wake, Merveille Bope baada ya kupata pasi murua kutoka kwa mchezaji mwenzake Roger Assale.

Mazembe walipata nafasi hiyo ya kipekee ya kupata bao baada ya mshambuliaji wake raia wa Tanzania, Thomas Ulimwengu kuangushwa katika eneo la hatari na refarii Janny Sikwaze kutoka Zambia kuwapa mkwaju wa adhabu.

Kwa matokeo haya, TP Mazembe inaendelea kuongoza kundi la A kwa alama 6, baada ya kushinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Medeama ya Ghana kwa mabao 3 kwa 1 wiki mbili zilizopita. Yanga haina alama yoyote kwa sababu mechi yake ya kwanza ilifungwa na Mo Bejaia ya Algeria bao 1 kwa 0.

Mechi ijayo Yanga wataikaribisha Medeama ya Ghana huku TP Mazembe ikisafiri kwenda ugenini kumenyana na MO Bejaia katikati ya mwezi ujao wa Julai.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com