Mbao FC yashushwa kileleni ligi kuu…


Baada ya Jana kuona watani wa Jadi Simba na Yanga wakitoshana nguvu kwenye mwendelezo wa lii kuu Tanzania bara , leo siku ya Jumatatu , Viwanja 6 vimewaka moto huku waliokua wakiongoza ligi hiyo , klabu ya Mbao FC ikiambulia kichapo cha goli . 1 – 0 dhidi ya Ruvu shooting na kuifanya kushushwa kutoka kileleni mwa ligi hiyo .

Bao la pekee la mchezo dhidi ya Mbao FC na Ruvu shooting liligungwa na Said Dilunga katika dakika ya 37 ya mchezo .

Katika michezo Mingine ,  Kikosi cha Coastal Union ya Tanga kimeichapa Mwadui FC bao 1-0, kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mkwakwani mkoani Tanga. Coastal union ilipata bao la kuongoza dakika 36, lililodumu hadi mwisho,  likiwekwa wavuni na Deogratius Anthony aliyeunganishiwa pasi ya Hassan Ali.

 

Mchezo mwingine ulizikutanisha timu za JKT Tanzania na African Lyon ambapo JKT Tanzania waliweza kuondoka na ushindi wa bao  1 – 0 , huku goli pekee la mchezo likiwekwa wavuni na Abdulrahman Mussa  dakika ya 56 .

 

Mtibwa Sugar iliweza kurudi  kileleni  mwa ligi kuu baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

 

Mchezo mwingine ulihusisha klabu ya  Mbeya City iliyoibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji Stand United Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com