Mbao FC yawafunga Yanga 1 – 0 na kutinga fainali kombe la shirikisho…


Mabingwa watetezi Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Yanga ,  wametolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kukubali kipigo cha bao 1- 0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mbao FC ambao walianza mchezo kwa kasi katika dakika za kwanza na kuwafanya kutengeneza nafasi kadhaa katika lango la Yanga, walifanikiwa kumuona mlinda mlango wa Yanga katika dakika ya 26 baada ya mchezaji wa Yanga Andrew Vicent kujifunga wakati akiokoa mpira katika lango lao.

Kufuatia mchezo huo mpaka wanakwenda mapumziko Mbao FC walikuwa wakiongoza kwa bao 1 dhidi ya Yanga bao ambalo limedumu mpaka dakika tisini za mchezo kwa Yanga kushindwa kusawazisha.

Hivyo Mbao FC sasa watakutana na Simba katika fainali ya kombe la Shirikisho ambao unatarajia kufanyika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com